Judges 1:22-27

22 aBasi nyumba ya Yusufu wakashambulia Betheli, naye Bwana alikuwa pamoja nao. 23 bWalipotuma watu kwenda kupeleleza Betheli (ambao hapo kwanza uliitwa Luzu), 24 cwale wapelelezi wakaona mtu anatoka mjini, nao wakamwambia, “Tuonyeshe jinsi ya kuingia mjini nasi tutakutendea wema.” 25 dHivyo akawaonyesha, nao wakaupiga mji kwa upanga lakini wakamhifadhi hai yule mtu na jamaa yake yote. 26 eYule mtu akaenda hadi nchi ya Wahiti, ambapo aliujenga mji na kuuita Luzu, ambao ndio jina lake hadi leo.

27 fLakini Manase hawakuwafukuza watu wa Beth-Shani na vijiji vyake, au watu wa Taanaki na vijiji vyake, au watu wa Dori na vijiji vyake, au watu wa Ibleamu na vijiji vyake, au watu wa Megido na vijiji vyake, lakini Wakanaani waliazimu kuishi katika nchi ile.
Copyright information for SwhKC